emblem

The United Republic of Tanzania

Tobacco Research Institute of Tanzania (TORITA)

Events

SEKTA YA TUMBAKU TANZANIA: ITIFAKI YA UZALISHAJI WA TUMBAKU KWA MSIMU WA MVUA ZA EL NIÑO KWA MWAKA 2026/27SEKTA YA TUMBAKU TANZANIA: ITIFAKI YA UZALISHAJI WA TUMBAKU KWA MSIMU WA MVUA ZA EL N


Imetolewa na TORITA tarehe 07 Septemba 2026 saa 1:30 asubuhi SEKTA YA TUMBAKU TANZANIA: ITIFAKI YA UZALISHAJI WA TUMBAKU KWA MSIMU WA MVUA ZA EL NIÑO KWA MWAKA 2026/27 “Sia mbegu za tumbaku mapema kwenye kitalu, hakikisha eneo la mizizi lina hewa ya kutosha, zuia upotevu wa virutubisho, zalisha miche imara, zingatia muda sahihi wa kupandikiza miche shambani, epuka kuongezeka kwa magonjwa, vuna majani yanapofikia ukomavu sahihi, na linda ubora wa majani wakati wa ukaushaji na utunzaji wa majani” Utabiri rasmi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) wa mvua za Vuli (Oktoba - Desemba 2026) unahusu maeneo ya Tanzania yenye misimu miwili ya mvua, ambayo ni ukanda wa Ziwa Victoria, Pwani ya Kaskazini, Nyanda za Juu Kaskazini-Mashariki na Kaskazini mwa Kigoma. TMA imesema maeneo haya yanatarajiwa kupata mvua za kiwango cha kawaida hadi juu ya kawaida, huku mvua zikitarajiwa kuanza mwishoni mwa Septemba/mapema Oktoba, pamoja na kuongezeka kwa hatari ya unyevu mwingi kwenye udongo na mafuriko. Mwezi Novemba 2026 unatarajiwa kuwa na ongezeko kubwa zaidi la mvua, na baadhi ya mvua zinaweza kuendelea hadi Januari 2027. Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania inaonya kuhusu athari kubwa za El Niño, unyevu mwingi kwenye udongo na uwezekano wa kutokea kwa mafuriko. Jedwali 1: Mtazamo wa jumla wa hali ya mvua kwa maeneo yalimayo tumbaku Eneo la tumbaku Jambo kuu la kuzingatia kwa msimu wa 2026/27 Hatua ya kuchukua Serengeti Uwezekano mkubwa wa mvua za Vuli/El Niño Andaa mifereji ya kutolea maji na kitalu kilichoinuliwa Geita Mvua kubwa na zinazoweza kuendelea kwa muda mrefu, pamoja na mafuriko Jiandae kwa mvua kubwa na mafuriko Kasulu Mvua kubwa na zinazoweza kuendelea kwa muda mrefu, pamoja na mafuriko Jiandae kwa mvua kubwa na mafuriko Kahama Fuatilia kwa karibu utabiri wa mvua Jiandae kwa mvua kubwa Tabora Kwa kiasi kikubwa ni eneo la uzalishaji linalotegemea msimu mmoja wa mvua Subiri utabiri mahsusi wa TMA kwa kipindi cha Novemba hadi Aprili Uyui Msimu mmoja wa mvua Fuatilia utabiri wa TMA wa siku 10 na wa kila mwezi na utabiri wa Novemba hadi Aprili Sikonge Msimu mmoja wa mvua Zingatia kwa ukaribu usimamizi wa mvua, udhibiti wa upotevu wa virutubisho shambani Urambo Msimu mmoja wa mvua Mipitisho ya maji pamoja na matumizi ya mbolea kwa awamu mbili au tatu ni muhimu sana Ulyankulu Mazingira ya uzalishaji ya msimu mmoja wa mvua Fuata ushauri wa TMA na maafisa ugani wa eneo husika Mpanda Msimu mmoja wa mvua Jiandae kwa vipindi vya mvua kubwa Manyoni Eneo lenye msimu mmoja wa mvua/na ukame Fuatilia muda wa kuanza na mtawanyiko wa mvua Chunya Mvua za msimu wa Novemba hadi Aprili Vipindi vya mvua kubwa vinaweza kutokea; andaa mifereji ya kupitisha maji Iringa Mvua za msimu Fuatilia mwanzo wa mvua na vipindi vya mvua kubwa kutoka TMA Songea Mvua za msimu wa Novemba hadi Aprili Fuatilia kwa karibu utabiri wa msimu wa mvua kutoka TMA Imetolewa na TORITA tarehe 07 Septemba 2026 saa 1:30 asubuhi Utofauti wa hapo juu ni muhimu kwa sababu utabiri wa sasa wa Mamlaka ya Hali ya Hewa kwa mvua za Vuli si utabiri unaohusu kila wilaya inayolima tumbaku nchini Tanzania. Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini unaeleza wazi kwamba utabiri wa mvua za Vuli ambao utaleta athari za mvua nyingi za El Nino unalenga hasa maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua. Kwa Tabora, Sikonge, Uyui, Urambo, Mpanda, Manyoni, Chunya, Songea na maeneo mengine yanayofanana, TORITA inashauri maeneo hayo kufuatilia kwa ukaribu utabiri wa mwezi wa Novemba 2026 hadi Aprili 2027 utakaotolewa, pamoja na utabiri wa hali ya hewa kwa kilimo wa siku 10 na wa kila mwezi kwa tahadhari. Hata hivyo, tahadhari dhidi ya El Niño inapaswa kuchukuliwa, kwa kuwa TMA hutoa utabiri wa kilimo kwa vipindi vya siku 10 na kwa msimu ili kusaidia katika mipango ya shughuli za kilimo. HATUA ZA KITAALAMU KUKABILI MVUA ZA EL NIÑO KWA UZALISHAJI WA TUMBAKU KWA MSIMU WA MWAKA 2026/27 KATIKA MAENEO YOTE YA TUMBAKU NCHINI TANZANIA 1. VITALU VYA MICHE YA TUMBAKU: hatua ya kwanza na muhimu kuzingatiwa TORITA tayari inapendekeza kwamba vitalu vya mbegu za tumbaku viwe vimeinuliwa na visiwekwe katika maeneo ya ulalo wa chini, vikiwa na udongo wenye rutuba, unaopitisha hewa vizuri na wenye kiasi kizuri cha masalia ya mimea (mboji). Kwa msimu wa El Niño, tunapendekeza kusisitiza zaidi ushauri ufuatao. A. Uinuaji wa vitalu vya tumbaku Msimu huu tunatarajia kuwa na mvua nyingi, katika hali hii, vitalu vya tumbaku viandaliwe kwa kutotoa fursa ya maji kutuama, hivyo vitalu viinuliwe kwa urefu wa sentimita 30 hadi 45, vikiwa na upana wa mita 1 kwa urefu wa mita 20 ili kuvihudumia kwa urahisi, badala ya kuwa na mwinuko wa sentimita 10 hadi 15 kama unaotumika wakati wa mvua za kawaida, ambapo kitalu cha kawaida huwa na upana wa mita 1.5 na urefu wa mita 20. Wakulima wanapaswa kuchagua eneo lililoinuka kwa ajili ya kuanzisha vitalu vya mbegu. Imetolewa na TORITA tarehe 07 Septemba 2026 saa 1:30 asubuhi Picha 1: Vitalu vilivyoinuliwa juu ili kuweza kutotuamisha maji B. Weka mifereji ya kupitisha maji kwenye kila kitalu Kitalu kilichoinuliwa juu pekee hakitoshi. Tunapendekeza kuweka nafasi ya njia ya mita 1 wenye mlalo ili kuruhusu maji kutoka kwenye kitalu badala ya kukusanyika kati ya vitalu, jambo ambalo linaweza kusababisha magonjwa ya ukungu (fangasi). TAHADHARI: Usiweke kitalu katika eneo la chini au linalotuamisha maji C. Epuka kumwagilia maji kupita kiasi Wakati wa mvua nyingi, lengo linabadilika kutoka kumwagilia maji hadi kudhibiti maji. Wakulima hawapaswi kumwagilia kwa kufuata ratiba ya kawaida. Umwagiliaji unapaswa kufanywa kwa kuzingatia kiasi halisi cha unyevu kilichopo kwenye udongo. E. Kukomaza miche kabla ya kupandikiza shambani Inafahamika kwamba kukatia majani ya miche (clipping) na kuikomaza miche (hardening) kabla ya kupandikiza shambani ni muhimu na vivyo hivyo kwa msimu wa mvua za El Niño, ambapo miche iliyokomazwa vizuri ni muhimu zaidi kwa kupandikizwa shambani, na ikiapndikizwa kwenye udongo wenye unyevu mwingi inaweza kusababisha mshtuko mkubwa kwa miche na kuongezeka kwa magonjwa. 2. KUPANDIKIZA MICHE: usiweke miche kwenye udongo uliojaa maji “Usipandikize miche mara moja baada ya mvua kubwa.” Pandikiza miche wakati udongo una unyevu wa kutosha lakini usiotuamisha maji. Dumisha nafasi ya mita 0.5 kati ya mimea na mita Imetolewa na TORITA tarehe 07 Septemba 2026 saa 1:30 asubuhi 1.2 kati ya matuta, pamoja na njia au mifereji ya maji ili kuhakikisha eneo la mizizi linabaki juu ya maji yanayoweza kutuama kwa muda. Picha 2: Matuta yaliyo na mifereji ya kupitisha maji 3. MBOLEA: hapa ndipo El Niño inaweza kusababisha upotevu mkubwa wa mbolea Mvua nyingi zinaweza kusababisha kuzamishwa chini ya udongo wenye mizizi kwa nitrojeni, potashamu, virutubisho kusombwa na maji, mizizi kushindwa kufyonza virutubisho ipasavyo, upungufu wa hewa kwenye udongo uliojaa maji na kusababisha upotevu wa virutubisho muhimu. Hivyo, kuongeza mbolea zaid kwa sababu mimea kuonekana kuwa dhaifu kunaweza kuwa hatari. i. Uwekaji mbolea ya kupandia kwenye mvua nyingi: Gawanya badala ya kuweka kiasi chote Weka kiasi kinachofaa cha mbolea katika eneo la mizizi na zingatia matumizi ya mbolea kwa kuweka awamu mbili hadi tatu, kutegemea hali ya hewa. Kwa mfano weka gramu 15 za mbolea kupandia kwa kila mche, kisha baada ya wiki mbili weka gramu 15 kwa kila mche; au weka gramu 10 kwa kila mche kila baada ya wiki mbili, kulingana na ushauri wa kitaalamu na hali ya shamba. Usiweke kiasi chote cha gramu 30 cha mbolea mara moja kabla ya kunyesha mvua kubwa iliyotabiriwa. TAHADHARI: Ikiwa Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) itatoa tahadhari ya mvua kubwa, ahirisha uwekaji wa mbolea hadi mvua kubwa imalizike kunyesha, pale ambapo kwa kitaalamu inawezekana. ii. Mbolea ya kukuzia: gawanya badala ya kuweka yote Weka mbolea katika eneo la mizizi na zingatia hali sahihi ya udongo na hali ya hewa kama ilivyoelezwa hapo juu Imetolewa na TORITA tarehe 07 Septemba 2026 saa 1:30 asubuhi 4. UONDOSHAJI WA MAJI SHAMBANI NI UTARATIBU WA KAWAIDA WAKATI WA EL NIÑO “Pasiwepo shamba la tumbaku linalopaswa kuwa na maji yaliyotuama kuzunguka eneo la mizizi ya tumbaku baada ya mvua kubwa.” Wakulima wanapaswa kutengeneza matuta kabla ya kupandikiza miche, kudumisha mifereji ya kutolea maji, kuondoa vizuizi kwenye mifereji ya maji, kuzuia maji yanayotoka kwenye mashamba jirani kuingia kwenye shamba la tumbaku, kutengeneza mifereji ya kugeuza maji pale inapohitajika, kuepuka kupanda tumbaku katika maeneo ya asili yanayotuamisha maji, kurekebisha mmomonyoko wa udongo mara moja baada ya mvua kubwa. Lengo si kuondoa maji yote shambani, bali kuondoa maji ya ziada kwa haraka huku ukihifadhi unyevu wa kutosha katika eneo la mizizi. 5. WADUDU NA MAGONJWA Hili linaweza kuwa mojawapo ya madhara makubwa yaliyofichika ya El Niño, kwa kuwa hali ya unyevu mwingi huongeza uwezekano wa magonjwa mengi ya fangasi na bakteria. Tafadhali toa taarifa kupitia ujumbe wa simu au WhatsApp kwenda namba 0787365585 mara tu unapobaini uwepo wa wadudu au magonjwa. Katika taarifa yako, toa taarifa ya eneo lako la shamba, Chama chako cha Msingi, Unioni yako, Kijiji, Wilaya na Mkoa. Hivyo, kagua vitalu kila siku, ondoa miche iliyoathirika mara moja, zuia miche iliyoambukizwa kupandikizwa shambani, epuka umwagiliaji kupita kiasi, dumisha nafasi sahihi kati ya mimea na uingizaji mzuri wa hewa, epuka kutembea bila sababu katika mashamba ya tumbaku yaliyo na unyevu, safisha na kuua vijidudu kwenye vifaa pale inapofaa, badilisha maeneo ya uzalishaji kwa misimu tofauti pale inapowezekana, tumia viuatilifu vya wadudu na magonjwa vilivyosajiliwa na kwa matumizi stahiki kwa kufuata maelekezo yaliyo kwenye lebo ya kiuatilifu. 6. UVUNAJI: usiache majani yaliyokomaa kuwa shambani kipindi cha mvua nyingi Mvua kubwa na nyingi zinapotabiriwa kagua mapema majani yaliyofikia ukomavu, panga vibarua mapema, vuna majani yaliyofikia ukomavu unaofaa kabla ya vipindi virefu vya mvua, kwa ubora wa tumbaku usiachie tumbaku iliyovunwa wazi kwenye mvua, peleka majani yaliyovunwa haraka kwenye bani kwa ukaushaji na epuka kurundika kwa kubanana majani yenye unyevu mwingi. 7. UKAUSHAJI: hili laweza kuwa eneo muhimu sana kuzingatiwa Mvua kubwa huleta changamoto kubwa kwenye bani la tumbaku kutokana na mchanganyiko wa: unyevu mwingi wa hewa + majani yenye unyevu + uingizaji hewa hafifu + ugumu wa kudhibiti hali ya ukaushaji. Imetolewa na TORITA tarehe 07 Septemba 2026 saa 1:30 asubuhi Hivyo, wakulima wanapaswa kuandaa na kukarabati mabani ya kukaushia tumbaku kabla mvua hazijaanza kunyesha. Maandalizi yanayopendekezwa kwenye bani ni pamoja na • Kurekebisha sehemu zinazovuja kwenye paa, kurekebisha milango na mifumo ya kudhibiti uingizaji hewa, hakikisha mvua haiwezi kuingia kupitia mianya, kagua vifaa vya kukaushia tumbaku kabla ya kuanza kuvuna, hakikisha kuna nishati ya kutosha ya kukaushia, sakafu iwe kavu, zuia majani yaliyovunwa yasigusane na sehemu zenye unyevu. • Usitumie ratiba maalumu ya ukaushaji bila kuzingatia hali ya hewa. Wakati wa hali ya kawaida ya hewa, wakulima wanaweza kuwa na ratiba inayotabirika ya ukaushaji. Wakati wa El Niño, joto na unyevunyevu ndani ya banda la kukaushia vinaweza kubadilika tofauti na hali ya kawaida. • Fuata ratiba ya ukaushaji kulingana na hali ya jani na vipimo vya hali ya ndani ya bani, si kwa kuzingatia muda uliopita pekee. Hivyo, inapowezekana, mabani ya kukaushia tumbaku yanapaswa kuwa na kipima joto, ifaa cha kupima unyevunyevu, mfumo wa kudhibiti uingizaji hewa na chanzo cha nishati ya joto cha kuaminika. 8. UTUNZAJI WA TUMBAKU: linda majani yalikaushwa kutopata unyevu Hatua hii ni muhimu sana baada ya ukaushaji. Ikiwa jani lililokaushwa likifyonza unyevu kutoka kwenye hewa yenye unyevunyevu, jani linaweza kupata ukungu na kushuka kwa ubora. Hivyo, hifadhi majani ya tumbaku katika chumba safi na kikavu, rekebisha sehemu zinazovuja kwenye paa na kuta, usiweke tumbaku moja kwa moja kwenye sakafu, tumia pallets/vitako vya kuhifadhia majani yaliyokaushwa pale inapowezekana, hakikisha kuta na sakafu vinabaki kuwa ni vikavu, zuia maji ya mvua kuingia kwenye chumba cha kuhifadhia majani ya tumbaku, epuka kubananisha sana majani yenye unyevu kupita kiasi, kagua mara kwa mara kama kuna ukungu au joto lisilo la kawaida na tenga mabelo yanayohisiwa kuwa na tatizo na yasichanganywe na tumbaku iliyo katika hali nzuri.

Imetolewa na TORITA tarehe 07 Septemba 2026 saa 1:30 asubuhi

SEKTA YA TUMBAKU TANZANIA: ITIFAKI YA UZALISHAJI WA TUMBAKU KWA MSIMU WA MVUA ZA EL NIÑO KWA MWAKA 2026/27

“Sia mbegu za tumbaku mapema kwenye kitalu, hakikisha eneo la mizizi lina hewa ya kutosha, zuia upotevu wa virutubisho, zalisha miche imara, zingatia muda sahihi wa kupandikiza miche shambani, epuka kuongezeka kwa magonjwa, vuna majani yanapofikia ukomavu sahihi, na linda ubora wa majani wakati wa ukaushaji na utunzaji wa majani”

Utabiri rasmi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) wa mvua za Vuli (Oktoba - Desemba 2026) unahusu maeneo ya Tanzania yenye misimu miwili ya mvua, ambayo ni ukanda wa Ziwa Victoria, Pwani ya Kaskazini, Nyanda za Juu Kaskazini-Mashariki na Kaskazini mwa Kigoma. TMA imesema maeneo haya yanatarajiwa kupata mvua za kiwango cha kawaida hadi juu ya kawaida, huku mvua zikitarajiwa kuanza mwishoni mwa Septemba/mapema Oktoba, pamoja na kuongezeka kwa hatari ya unyevu mwingi kwenye udongo na mafuriko. Mwezi Novemba 2026 unatarajiwa kuwa na ongezeko kubwa zaidi la mvua, na baadhi ya mvua zinaweza kuendelea hadi Januari 2027. Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania inaonya kuhusu athari kubwa za El Niño, unyevu mwingi kwenye udongo na uwezekano wa kutokea kwa mafuriko.

Jedwali 1: Mtazamo wa jumla wa hali ya mvua kwa maeneo yalimayo tumbaku Eneo la tumbaku

Jambo kuu la kuzingatia kwa msimu wa 2026/27

Hatua ya kuchukua

Serengeti

Uwezekano mkubwa wa mvua za Vuli/El Niño

Andaa mifereji ya kutolea maji na kitalu kilichoinuliwa

Geita

Mvua kubwa na zinazoweza kuendelea kwa muda mrefu, pamoja na mafuriko

Jiandae kwa mvua kubwa na mafuriko

Kasulu

Mvua kubwa na zinazoweza kuendelea kwa muda mrefu, pamoja na mafuriko

Jiandae kwa mvua kubwa na mafuriko

Kahama

Fuatilia kwa karibu utabiri wa mvua

Jiandae kwa mvua kubwa

Tabora

Kwa kiasi kikubwa ni eneo la uzalishaji linalotegemea msimu mmoja wa mvua

Subiri utabiri mahsusi wa TMA kwa kipindi cha Novemba hadi Aprili

Uyui

Msimu mmoja wa mvua

Fuatilia utabiri wa TMA wa siku 10 na wa kila mwezi na utabiri wa Novemba hadi Aprili

Sikonge

Msimu mmoja wa mvua

Zingatia kwa ukaribu usimamizi wa mvua, udhibiti wa upotevu wa virutubisho shambani

Urambo

Msimu mmoja wa mvua

Mipitisho ya maji pamoja na matumizi ya mbolea kwa awamu mbili au tatu ni muhimu sana

Ulyankulu

Mazingira ya uzalishaji ya msimu mmoja wa mvua

Fuata ushauri wa TMA na maafisa ugani wa eneo husika

Mpanda

Msimu mmoja wa mvua

Jiandae kwa vipindi vya mvua kubwa

Manyoni

Eneo lenye msimu mmoja wa mvua/na ukame

Fuatilia muda wa kuanza na mtawanyiko wa mvua

Chunya

Mvua za msimu wa Novemba hadi Aprili

Vipindi vya mvua kubwa vinaweza kutokea; andaa mifereji ya kupitisha maji

Iringa

Mvua za msimu

Fuatilia mwanzo wa mvua na vipindi vya mvua kubwa kutoka TMA

Songea

Mvua za msimu wa Novemba hadi Aprili

Fuatilia kwa karibu utabiri wa msimu wa mvua kutoka TMA

Imetolewa na TORITA tarehe 07 Septemba 2026 saa 1:30 asubuhi

Utofauti wa hapo juu ni muhimu kwa sababu utabiri wa sasa wa Mamlaka ya Hali ya Hewa kwa mvua za Vuli si utabiri unaohusu kila wilaya inayolima tumbaku nchini Tanzania. Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini unaeleza wazi kwamba utabiri wa mvua za Vuli ambao utaleta athari za mvua nyingi za El Nino unalenga hasa maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua.

Kwa Tabora, Sikonge, Uyui, Urambo, Mpanda, Manyoni, Chunya, Songea na maeneo mengine yanayofanana, TORITA inashauri maeneo hayo kufuatilia kwa ukaribu utabiri wa mwezi wa Novemba 2026 hadi Aprili 2027 utakaotolewa, pamoja na utabiri wa hali ya hewa kwa kilimo wa siku 10 na wa kila mwezi kwa tahadhari. Hata hivyo, tahadhari dhidi ya El Niño inapaswa kuchukuliwa, kwa kuwa TMA hutoa utabiri wa kilimo kwa vipindi vya siku 10 na kwa msimu ili kusaidia katika mipango ya shughuli za kilimo.

HATUA ZA KITAALAMU KUKABILI MVUA ZA EL NIÑO KWA UZALISHAJI WA TUMBAKU KWA MSIMU WA MWAKA 2026/27 KATIKA MAENEO YOTE YA TUMBAKU NCHINI TANZANIA

1. VITALU VYA MICHE YA TUMBAKU: hatua ya kwanza na muhimu kuzingatiwa

TORITA tayari inapendekeza kwamba vitalu vya mbegu za tumbaku viwe vimeinuliwa na visiwekwe katika maeneo ya ulalo wa chini, vikiwa na udongo wenye rutuba, unaopitisha hewa vizuri na wenye kiasi kizuri cha masalia ya mimea (mboji).

Kwa msimu wa El Niño, tunapendekeza kusisitiza zaidi ushauri ufuatao.

A. Uinuaji wa vitalu vya tumbaku

Msimu huu tunatarajia kuwa na mvua nyingi, katika hali hii, vitalu vya tumbaku viandaliwe kwa kutotoa fursa ya maji kutuama, hivyo vitalu viinuliwe kwa urefu wa sentimita 30 hadi 45, vikiwa na upana wa mita 1 kwa urefu wa mita 20 ili kuvihudumia kwa urahisi, badala ya kuwa na mwinuko wa sentimita 10 hadi 15 kama unaotumika wakati wa mvua za kawaida, ambapo kitalu cha kawaida huwa na upana wa mita 1.5 na urefu wa mita 20. Wakulima wanapaswa kuchagua eneo lililoinuka kwa ajili ya kuanzisha vitalu vya mbegu.

Imetolewa na TORITA tarehe 07 Septemba 2026 saa 1:30 asubuhi

Picha 1: Vitalu vilivyoinuliwa juu ili kuweza kutotuamisha maji

B. Weka mifereji ya kupitisha maji kwenye kila kitalu

Kitalu kilichoinuliwa juu pekee hakitoshi. Tunapendekeza kuweka nafasi ya njia ya mita 1 wenye mlalo ili kuruhusu maji kutoka kwenye kitalu badala ya kukusanyika kati ya vitalu, jambo ambalo linaweza kusababisha magonjwa ya ukungu (fangasi).

TAHADHARI: Usiweke kitalu katika eneo la chini au linalotuamisha maji

C. Epuka kumwagilia maji kupita kiasi

Wakati wa mvua nyingi, lengo linabadilika kutoka kumwagilia maji hadi kudhibiti maji. Wakulima hawapaswi kumwagilia kwa kufuata ratiba ya kawaida. Umwagiliaji unapaswa kufanywa kwa kuzingatia kiasi halisi cha unyevu kilichopo kwenye udongo.

E. Kukomaza miche kabla ya kupandikiza shambani

Inafahamika kwamba kukatia majani ya miche (clipping) na kuikomaza miche (hardening) kabla ya kupandikiza shambani ni muhimu na vivyo hivyo kwa msimu wa mvua za El Niño, ambapo miche iliyokomazwa vizuri ni muhimu zaidi kwa kupandikizwa shambani, na ikiapndikizwa kwenye udongo wenye unyevu mwingi inaweza kusababisha mshtuko mkubwa kwa miche na kuongezeka kwa magonjwa.

2. KUPANDIKIZA MICHE: usiweke miche kwenye udongo uliojaa maji

“Usipandikize miche mara moja baada ya mvua kubwa.” Pandikiza miche wakati udongo una unyevu wa kutosha lakini usiotuamisha maji. Dumisha nafasi ya mita 0.5 kati ya mimea na mita

Imetolewa na TORITA tarehe 07 Septemba 2026 saa 1:30 asubuhi

1.2 kati ya matuta, pamoja na njia au mifereji ya maji ili kuhakikisha eneo la mizizi linabaki juu ya maji yanayoweza kutuama kwa muda.

Picha 2: Matuta yaliyo na mifereji ya kupitisha maji

3. MBOLEA: hapa ndipo El Niño inaweza kusababisha upotevu mkubwa wa mbolea

Mvua nyingi zinaweza kusababisha kuzamishwa chini ya udongo wenye mizizi kwa nitrojeni, potashamu, virutubisho kusombwa na maji, mizizi kushindwa kufyonza virutubisho ipasavyo, upungufu wa hewa kwenye udongo uliojaa maji na kusababisha upotevu wa virutubisho muhimu. Hivyo, kuongeza mbolea zaid kwa sababu mimea kuonekana kuwa dhaifu kunaweza kuwa hatari.

i. Uwekaji mbolea ya kupandia kwenye mvua nyingi: Gawanya badala ya kuweka kiasi chote

Weka kiasi kinachofaa cha mbolea katika eneo la mizizi na zingatia matumizi ya mbolea kwa kuweka awamu mbili hadi tatu, kutegemea hali ya hewa. Kwa mfano weka gramu 15 za mbolea kupandia kwa kila mche, kisha baada ya wiki mbili weka gramu 15 kwa kila mche; au weka gramu 10 kwa kila mche kila baada ya wiki mbili, kulingana na ushauri wa kitaalamu na hali ya shamba. Usiweke kiasi chote cha gramu 30 cha mbolea mara moja kabla ya kunyesha mvua kubwa iliyotabiriwa.

TAHADHARI: Ikiwa Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) itatoa tahadhari ya mvua kubwa, ahirisha uwekaji wa mbolea hadi mvua kubwa imalizike kunyesha, pale ambapo kwa kitaalamu inawezekana.

ii. Mbolea ya kukuzia: gawanya badala ya kuweka yote

Weka mbolea katika eneo la mizizi na zingatia hali sahihi ya udongo na hali ya hewa kama ilivyoelezwa hapo juu

Imetolewa na TORITA tarehe 07 Septemba 2026 saa 1:30 asubuhi

4. UONDOSHAJI WA MAJI SHAMBANI NI UTARATIBU WA KAWAIDA WAKATI WA EL NIÑO

“Pasiwepo shamba la tumbaku linalopaswa kuwa na maji yaliyotuama kuzunguka eneo la mizizi ya tumbaku baada ya mvua kubwa.”

Wakulima wanapaswa kutengeneza matuta kabla ya kupandikiza miche, kudumisha mifereji ya kutolea maji, kuondoa vizuizi kwenye mifereji ya maji, kuzuia maji yanayotoka kwenye mashamba jirani kuingia kwenye shamba la tumbaku, kutengeneza mifereji ya kugeuza maji pale inapohitajika, kuepuka kupanda tumbaku katika maeneo ya asili yanayotuamisha maji, kurekebisha mmomonyoko wa udongo mara moja baada ya mvua kubwa. Lengo si kuondoa maji yote shambani, bali kuondoa maji ya ziada kwa haraka huku ukihifadhi unyevu wa kutosha katika eneo la mizizi.

5. WADUDU NA MAGONJWA

Hili linaweza kuwa mojawapo ya madhara makubwa yaliyofichika ya El Niño, kwa kuwa hali ya unyevu mwingi huongeza uwezekano wa magonjwa mengi ya fangasi na bakteria.

Tafadhali toa taarifa kupitia ujumbe wa simu au WhatsApp kwenda namba 0787365585 mara tu unapobaini uwepo wa wadudu au magonjwa. Katika taarifa yako, toa taarifa ya eneo lako la shamba, Chama chako cha Msingi, Unioni yako, Kijiji, Wilaya na Mkoa.

Hivyo, kagua vitalu kila siku, ondoa miche iliyoathirika mara moja, zuia miche iliyoambukizwa kupandikizwa shambani, epuka umwagiliaji kupita kiasi, dumisha nafasi sahihi kati ya mimea na uingizaji mzuri wa hewa, epuka kutembea bila sababu katika mashamba ya tumbaku yaliyo na unyevu, safisha na kuua vijidudu kwenye vifaa pale inapofaa, badilisha maeneo ya uzalishaji kwa misimu tofauti pale inapowezekana, tumia viuatilifu vya wadudu na magonjwa vilivyosajiliwa na kwa matumizi stahiki kwa kufuata maelekezo yaliyo kwenye lebo ya kiuatilifu.

6. UVUNAJI: usiache majani yaliyokomaa kuwa shambani kipindi cha mvua nyingi

Mvua kubwa na nyingi zinapotabiriwa kagua mapema majani yaliyofikia ukomavu, panga vibarua mapema, vuna majani yaliyofikia ukomavu unaofaa kabla ya vipindi virefu vya mvua, kwa ubora wa tumbaku usiachie tumbaku iliyovunwa wazi kwenye mvua, peleka majani yaliyovunwa haraka kwenye bani kwa ukaushaji na epuka kurundika kwa kubanana majani yenye unyevu mwingi.

7. UKAUSHAJI: hili laweza kuwa eneo muhimu sana kuzingatiwa

Mvua kubwa huleta changamoto kubwa kwenye bani la tumbaku kutokana na mchanganyiko wa:

unyevu mwingi wa hewa + majani yenye unyevu + uingizaji hewa hafifu + ugumu wa kudhibiti hali ya ukaushaji.

Imetolewa na TORITA tarehe 07 Septemba 2026 saa 1:30 asubuhi

Hivyo, wakulima wanapaswa kuandaa na kukarabati mabani ya kukaushia tumbaku kabla mvua hazijaanza kunyesha.

Maandalizi yanayopendekezwa kwenye bani ni pamoja na

  • Kurekebisha sehemu zinazovuja kwenye paa, kurekebisha milango na mifumo ya kudhibiti uingizaji hewa, hakikisha mvua haiwezi kuingia kupitia mianya, kagua vifaa vya kukaushia tumbaku kabla ya kuanza kuvuna, hakikisha kuna nishati ya kutosha ya kukaushia, sakafu iwe kavu, zuia majani yaliyovunwa yasigusane na sehemu zenye unyevu.

  • Usitumie ratiba maalumu ya ukaushaji bila kuzingatia hali ya hewa. Wakati wa hali ya kawaida ya hewa, wakulima wanaweza kuwa na ratiba inayotabirika ya ukaushaji. Wakati wa El Niño, joto na unyevunyevu ndani ya banda la kukaushia vinaweza kubadilika tofauti na hali ya kawaida.

  • Fuata ratiba ya ukaushaji kulingana na hali ya jani na vipimo vya hali ya ndani ya bani, si kwa kuzingatia muda uliopita pekee. Hivyo, inapowezekana, mabani ya kukaushia tumbaku yanapaswa kuwa na kipima joto, ifaa cha kupima unyevunyevu, mfumo wa kudhibiti uingizaji hewa na chanzo cha nishati ya joto cha kuaminika.

    8. UTUNZAJI WA TUMBAKU: linda majani yalikaushwa kutopata unyevu

    Hatua hii ni muhimu sana baada ya ukaushaji. Ikiwa jani lililokaushwa likifyonza unyevu kutoka kwenye hewa yenye unyevunyevu, jani linaweza kupata ukungu na kushuka kwa ubora.

    Hivyo, hifadhi majani ya tumbaku katika chumba safi na kikavu, rekebisha sehemu zinazovuja kwenye paa na kuta, usiweke tumbaku moja kwa moja kwenye sakafu, tumia pallets/vitako vya kuhifadhia majani yaliyokaushwa pale inapowezekana, hakikisha kuta na sakafu vinabaki kuwa ni vikavu, zuia maji ya mvua kuingia kwenye chumba cha kuhifadhia majani ya tumbaku, epuka kubananisha sana majani yenye unyevu kupita kiasi, kagua mara kwa mara kama kuna ukungu au joto lisilo la kawaida na tenga mabelo yanayohisiwa kuwa na tatizo na yasichanganywe na tumbaku iliyo katika hali nzuri.