emblem

The United Republic of Tanzania

Tobacco Research Institute of Tanzania (TORITA)

News

SIKUKUU YA WAKULIMA NANENANE 2023 ILIYOFANYIKA KITAIFA KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI KATIKA UWANJA WA JOHN MWAKANGALE JIJINI MBEYA


  • TAARIFA YA USHINDANISHAJI WA MAKUNDI MBALIMBALI NDANI NA NJE YA UWANJA KATIKA MAONESHO NA SIKUKUU YA WAKULIMA NANENANE 2023 ILIYOFANYIKA KITAIFA KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI KATIKA UWANJA WA JOHN MWAKANGALE JIJINI MBEYA
  • 1.0 Utangulizi
  • Maonesho na Sherehe ya Nanenane mwaka 2023 yamefanyika katika uwanja wa John B. Mwakangale Jijini Mbeya. Katika maonesho hayo waoneshaji walioshiriki ni 574 wakijumuishaWizara, Taasisi za Umma na binafsi, Asasi za Kiraia, Wabia wa Maendeleo, Makampuni,Taasisi za kifedha, wakulima, wafugaji, wavuvina waonaji walioshiriki wanakadiriwa kuwa zaidi ya 500,000.
  • Aidha, Maonesho na Sherehe ya Nanenane hupambwa naushindanishaji wa wadau wa Sekta za Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Ushirika na Washindi kupewa zawadi mbalimbali. Mashindano ya Nanenane hufanyika kwa kuzingatia Mwongozo wa Nanenane wa mwaka 2017 uliotolewa na Wizara ya Kilimo ambao unaainisha vigezo vya ushindanishaji kwa kila kundi ili kuhakikisha kwamba kunakuwa na usawa na haki.
  • 2.0 Wadau walioshindanishwa ndani na nje ya uwanja wa maonesho ni pamoja na;
  • 2.1 Wakulima wa mazao mbalimbali
  • 2.2 Wafugaji wa ng’ombe wa Maziwa
  • 2.3 Wafugaji wa ng’ombe wa Nyama
  • 2.4 Wafugaji wa Samaki/Kuku
  • 2.5 Vyama vya Ushirika
  • 2.6 Halmashauri
  • 2.7 Wizara, Taasisi na Makampuni ya umma na binafsi katika mnyororo wa thamani wa mazao ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi.
  • 3.0 Zoezi la ushindanishaji
  • Katika maonesho na sherehe za wakulima Nanenane mwaka 2023 Ushindanishaji wa wadau ulifanyika katika ngazi za Halmashauri, Mikoa, Kanda na hatimae kupata washindi ngazi ya Taifa.
  • Ushindanishajiulizingatia vigezo vya ushindanishaji ambavyo kwa kiasi kikubwa huzingatia ufanisi wa Halmashauri katika usimamizi na uendelezaji wa Sekta za Kilimo,Mifugo na Uvuvi ikiwemo matumizi ya teknolojia, kuongezeka kwa tija na uongezaji wa thamani. Aidha, mashindano ndani ya uwanja huzingatia vigezo mbalimbali vilivyowekwa vikiwemo mpangilio wa bidhaa, ubunifu na uwezo wa waoneshaji katika kueleza kwa ufasaha teknlojia inayooneshwa na kaulimbiu.
  • Sekretarieti ngazi ya Kanda ilianza rasmi kazi ya ushindanishaji ili kupata Washindi ngazi ya Taifa mnamo tarehe 23 Julai, 2023 kwa kutembelea Mikoa yote ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, ambapo ilitembelea na kufanikiwa kushindanisha Halmashauri kumi na nne (14), Wakulima 7, Wafugaji 18 katika makundi ya ng’ombe wa maziwa, ng’ombe wa nyama, kuku na samaki pamoja na Vyama vya Ushirika 7. Aidha, ushindanishaji wa Wakulima, Wafugaji na Vyama vya Ushirika ulifanyika kwa kutembelea maeneo wanayofanyia shughuli zao na kuhojiana nao ana kwa ana kwa kutumia vigezo vya ushindanishaji vya Nanenane.
  • Ushindanishaji wa makundi mbalimbali ndani ya uwanja umefanyika kuanzia tarehe 01 hadi 06 Agosti, 2023. Ushindanishaji huu ni kwa kuzingatia vigezo vya ushindanishaji wa Nanenane.
  • 4.0 Washindi katika Tasnia mbalimbali za Kilimo
  • Washindi wa Kitaifa wa makundi mbalimbali katika Sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi walipatikana kupitia Bodi za mazao ya Kilimo na Sekretarieti ya Maonesho ya Kitaifa kama ifuatavyo;
  • 4.1 Washindi ngazi ya Taifa
  • i)Kundi la Wakulima
  • Na. Jina Zao Halmashauri Mkoa Zawadi Imetolewa na:-
    1 Frank Timoth Msuya Parachichi Njombe TC Njombe Fedha Taslimu Sh.8,000,000 Sekretarieti ya Maonesho Kitaifa
    2 Japhet Tomasi Ngimbusi Mahindi Iringa DC Iringa Fedha Taslimu Sh.6,000,000 Sekretarieti ya Maonesho Kitaifa
    3 JamesChiwalanje Siame Mahindi Kalambo DC Rukwa Fedha Taslimu Sh. 4,000,000 Sekretarieti ya Maonesho Kitaifa
    4 Azam Abdelehemani Mfaume Korosho Masasi DC Mtwara Fedha Taslimu Sh.2,000,000 na bomba la kupulizia Mikorosho lenye thamani ya Sh.1,200,000 Bodi ya Korosho
    5. Simon Chambala Helahela Tumbaku Chunya Mbeya Fedha Taslimu Sh. 1,000,000.00 Bodi ya Tumbaku Tanzania
  • ii)Kundi la Wafugaji wa Ng’ombe wa Maziwa Kitaifa
  • Na. Jina Zao Halmashauri Mkoa Zawadi Imetolewa na:-
    1. Joinedi Dickson Mwashamba Ng’ombe wa maziwa Mbeya Jiji Mbeya Fedha taslimu Sh. 8,000,000 Sekretarieti ya Maonesho Kitaifa
    2 Amrani Wilion Mkakanzi Ng’ombe wa Maziwa Mufindi DC Iringa Fedha taslimu Sh. 6,000,000 Sekretarieti ya Maonesho Kitaifa
    3 Daina George Mangula Ng’ombe wa maziwa Njombe DC Njombe Fedha taslimu Sh. 4,000,000 Sekretarieti ya Maonesho Kitaifa
  • iii)Kundi la Wafugaji wa Ng’ombe wa Nyama Kitaifa
  • Na. Jina Zao Halmashauri Mkoa Zawadi Imetolewa na:-
    1 Beda Lucas Chipamba Ng’ombe wa nyama Kalambo DC Rukwa Fedha taslimu Sh. 8,000,000 Sekretarieti ya Maonesho Kitaifa
    2 Chuki Jeremia Mbwanjile Ng’ombe wa nyama Mbarali DC Mbeya Fedha taslimu Sh. 6,000,000 Sekretarieti ya Maonesho Kitaifa
    3 Hosea Kyando Ng’ombe wa nyama Mlele DC Katavi Fedha taslimu Sh. 4,000,000 Sekretarieti ya Maonesho Kitaifa
  • iv)Kundi la Wafugaji wa Samaki/Kuku
  • Na. Jina Zao Halmashauri Mkoa Zawadi Imetolewa na:-
    1 Filbert MaikoMasawe Kuku Sumbawanga Manispaa Rukwa Fedha taslimu Sh. 8,000,000 Sekretarieti ya Maonesho Kitaifa
    2 LoginusMgani Samaki Ludewa DC Njombe Fedha taslimu Sh. 6,000,000 Sekretarieti ya Maonesho Kitaifa
    3 Karolo Adolph Ndalamwigogo Kuku Mpanda Manispaa Katavi Fedha taslimu Sh. 4,000,000 Sekretarieti ya Maonesho Kitaifa
  • v)Kundi la Vyama vya Ushirika
  • Na. Jina Zao Halmashauri Mkoa Zawadi Imetolewa na:-
    1 IGAMBAMPYA AMCOS Kahawa MboziDC Songwe Trophy kubwa Sekretarieti ya Maonesho Kitaifa
    2 NKONDWE AMCOS Mboga mboga Mpanda MC Katavi Trophy ya kati Sekretarieti ya Maonesho Kitaifa
    3 MPUI AMCOS Mahindi Sumbawanga DC Rukwa Trophy ndogo Sekretarieti ya Maonesho Kitaifa
  • vi)Kundi la Halmashauri Kitaifa
  • Na. Halmashauri Mkoa Zawadi Imetolewa na:-
    1 LudewaDC NJOMBE Trophy kubwa Sekretarieti ya Maonesho Kitaifa
    2 Iringa MC IRINGA Trophy ya kati Sekretarieti ya Maonesho Kitaifa
    3 IringaDC IRINGA Trophy ndogo Sekretarieti ya Maonesho Kitaifa
  • 4.2.ORODHA YA WASHINDI WA JUMLA - TAASISI MBALIMBALI NANENANE – 2023
  • i)KUNDI LA WIZARA
  • NA JINA LA MSHINDI NAFASI
    1 WIZARA YA KILIMO Kwanza
    2 WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI Pili
    3 WIZARA YA FEDHA Tatu
  • ii)KUNDI LA WAKALA WA PEMBEJEO - VYETI
  • NA JINA LA MSHINDI NAFASI
    1 AFRIFARM Kwanza
    2 SNW POSITIVE INTERNATINAL Pili
    3 BAJUTA INTERNATIONAL TANZANIA Tatu
  • iii)KUNDI LA TAASISI ZA UDHIBITI UBORA NA VIWANGO
  • NA JINA LA MSHINDI NAFASI
    1 BOT Kwanza
    2 TFRA Pili
    3 TCRA Tatu
  • iv)KUNDI LA WAZALISHAJI/WASAMBAZJI MBEGU(Kilimo, Mifugo na Uvuvi)
  • NA JINA LA MSHINDI NAFASI
    1 SEEDCO Kwanza
    2 ASA(WAKALA WA MBEGU TANZANIA) Pili
    3 KIBO SEEDS Tatu
  • v)KUNDI LA BODI ZA MAZAO
  • NA JINA LA MSHINDI NAFASI
    1 BODI YA SUKARI TANZANIA Kwanza
    2 BODI YA NAFAKA NA MAZAO MCHANGANYIKO Pili
    3 BODI YA KAHAWA TANZANIA Tatu
  • vi)KUNDI LA TAASISI ZA FEDHA
  • NA JINA LA MSHINDI NAFASI
    1 CRDBBANK Kwanza
    2 NMB BANK Pili
    3 AZANIA BANK Tatu
  • vii)KUNDI LA KAMPUNI ZA UTANGAZAJI
  • NA JINA LA MSHINDI NAFASI
    1 TBC Kwanza
    2 ACCESS FM Pili
    3 HIGHLAND FM Tatu
  • viii)KUNDI LA WATENGENEZAJI/WASAMBAZAJI WA VINYWAJI
  • NA JINA LA MSHINDI NAFASI
    1 COCACOLA Kwanza
    2 SBS - PEPSI Pili
    3 MAT SUPER BRAND LIMITED Tatu
  • ix)KUNDI LA WAUZAJI WA ZANA ZA KILIMO
  • NA JINA LA MSHINDI NAFASI
    1 AGRICOM Kwanza
    2 POLYMACHINERY Pili
    3 SAGRA MOTOR COPERATION Tatu
  • x)KUNDI LA KAMPUNI ZA MAWASILIANO
  • NA JINA LA MSHINDI NAFASI
    1 VODACOM TANZANIA Kwanza
    2 TIGO TANZANIA Pili
    3 TTCL Tatu
  • xi)KUNDI LA WASINDIKAJI/WACHAKATAJI WA MAZAO YA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI
  • NA JINA LA MSHINDI NAFASI
    1 ASAS DAIRIES LTD Kwanza
    2 RAPHAEL GROUP Pili
    3 KHEBANDZA MARKETING Tatu
  • xii)KUNDI LA TAASISI ZA KIJESHI
  • NA JINA LA MSHINDI NAFASI
    1 JKT Kwanza
    2 MAGEREZA Pili
    3 POLISI Tatu
  • xiii)KUNDI LA TAASISI ZA UWEZESHAJI MIKOPO(KILIMO, MIFUGO NA UVUVI)
  • NA JINA LA MSHINDI NAFASI
    1 PASS Kwanza
    2 AMDT Pili
    3 MFUKO WA TAIFA WA PEMBEJEO Tatu
  • xiv)KUNDI LA ASASI ZA KIRAIA
  • NA JINA LA MSHINDI NAFASI
    1 TAHA Kwanza
    2 TWCC Pili
    3 SAGCOT Tatu
  • xv)KUNDI LA KUTOA HUDUMA ZA BIMA
  • NA JINA LA MSHINDI NAFASI
    1 NATIONAL INSUARANCE COPERATION Kwanza
    2 ZANZIBAR INSURANCE Pili
    3 JUBILEE GENERAL INSUARANCE Tatu
  • xvi)KUNDI LA TAASISI ZA ELIMU
  • NA JINA LA MSHINDI NAFASI
    1 CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM Kwanza
    2 MAT UYOLE Pili
    3 VETA Tatu
  • xvii)KUNDI LA TAASISI ZA UTAFITI WA KILIMO
  • NA JINA LA MSHINDI NAFASI
    1 TARI Kwanza
    2 TaCRI Pili
    3 TAFIRI Tatu
  • xviii)KUNDI LA WATOA HUDUMA ZA AFYA
  • NA JINA LA MSHINDI NAFASI
    1 HOSPITALI YA RUFAA KANDA YA MBEYA Kwanza
    2 HOSPITALI BENJAMIN MKAPA Pili
    3 HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA MBEYA Tatu
  • xix)KUNDI LA MAKAMPUNI YA UTENGENEZAJI/USAMBAZAJI WA MBOLEA
  • NA JINA LA MSHINDI NAFASI
    1 YARA TANZANIA Kwanza
    2 ETG Pili
    3 MINJINGU Tatu
  • XX) MSHINDI WA BANDA
  • BANDA BORA AGRICOM
  • 4.3.Washindi katika Mikoa ya Kanda
  • i)Kundi la Wakulima
  • Na. Jina Zao Halmashauri Mkoa Zawadi Imetolewa na:-
    1 EliasCharles Kyando Mahindi Tunduma TC Songwe Fedha taslimu Sh. 2,000,000 Sekretarieti ya Maonesho Kitaifa
    2 LusekeloMwakibete Parachichi Busokelo DC Mbeya Fedha taslimu Sh. 2,000,000 Sekretarieti ya Maonesho Kitaifa
    3 Magagi Miligwa Matanga Mahindi Mpimbwe DC Katavi Fedha taslimu Sh. 2,000,000 Sekretarieti ya Maonesho Kitaifa
    4 Kassian Haule Kahawa Mbinga TC Ruvuma Fedha taslimu Sh. 2,000,000 Sekretarieti ya Maonesho Kitaifa
  • ii)Kundi la Wafugaji wa Ng’ombe wa Maziwa
  • Na. Jina Zao Halmashauri Mkoa Zawadi Imetolewa na:-
    1 JaneSingo Ng’ombe wa Maziwa S/wanga MC Rukwa Fedha taslimu Sh. 2,000,000 Sekretarieti ya Maonesho Kitaifa
    2 Inocent Patrick Kimathy Ng’ombe wa Maziwa Mpanda MC Katavi Fedha taslimu Sh. 2,000,000 Sekretarieti ya Maonesho Kitaifa
    3 Agatha Christian Matembo Ng’ombe wa Maziwa Mbinga TC Ruvuma Fedha taslimu Sh. 2,000,000 Sekretarieti ya Maonesho Kitaifa
  • iii)Kundi la Wafugaji wa Ng’ombe wa Nyama
  • Na. Jina Zao Halmashauri Mkoa Zawadi Imetolewa na:-
    1 Yonel Timu Kyando Ng’ombe wa nyama Mbozi DC Songwe Fedha taslimu Sh. 2,000,000 Sekretarieti ya Maonesho Kitaifa
    2. Matambile Mgemaa Lemkamilo Ng’ombe wa nyama Iringa DC Iringa Fedha taslimu Sh. 2,000,000 Sekretarieti ya Maonesho Kitaifa
  • iv)Kundi la Wafugaji wa Samaki/Kuku
  • Na. Jina Zao Halmashauri Mkoa Zawadi Imetolewa na:-
    1 Dostea Seth Ngwema Samaki Mufindi DC Iringa Fedha taslimu Sh. 2,000,000 Sekretarieti ya Maonesho Kitaifa
    2 Upendo L. Mwanjala Samaki Rungwe DC Mbeya Fedha taslimu Sh. 2,000,000 Sekretarieti ya Maonesho Kitaifa
    3 Jesca Jackson Mwenda Samaki Mbozi DC Songwe Fedha taslimu Sh. 2,000,000 Sekretarieti ya Maonesho Kitaifa
    4 Omary Hassan Kalambo Samaki Songea DC Ruvuma Fedha taslimu Sh. 2,000,000 Sekretarieti ya Maonesho Kitaifa
  • 4.4 Zawadi kwa mikoa mitano(5) yenye uzalishaji mkubwa wa mazao ya kilimo msimu 2022/23 (Zawadi itatolewa na Wizara ya Kilimo)
  • 4.5 Tuzo/Shukrani mbalimbali
  • 4.5.1 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia SuluhuHassan toka kwa wananchi wa Mikoa ya Nyanda za Juuu Kusini kwa Mchango wake kubwa katika za kilimo, mifugo na uvuvi.
  • 4.5.2 Mdhamini mkuu, wadhamini wa kati na wachangiaji wengine
  • 4.5.3 Shukrani kwa Wizara za kisekta na Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini
  • 4.5.4 Vyeti kwa Makampuni ya Mkwawa, VOEDSEL na PREMIUM (Zawadi itatolewa na TORITA)